Kombe la Dunia la FIFA 2022

Kombe la Dunia 2022

Kombe la Dunia la FIFA 2022 (kwa Kiarabu :كَأسُ اَلعَالَمِ] 2022, Gulf Arabic: كَاسُ اَلعَالَمِ ٢٠٢٢) ni michuano ya 22 ya Kombe la Dunia la FIFA inayohusisha timu za taifa za wanaume kutoka mataifa mbalimbali katika mchezo wa soka. Michuano hii inashirikisha timu za wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa FIFA na hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. Michuano hii imepangwa kufanyika Qatar kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022[1].

Hili litakuwa Kombe la Dunia la kwanza kufanyika katika nchi za Kiarabu[2] na litakuwa Kombe la Dunia la pili kufanyika katika bara la Asia baada ya mashindano ya 2002 kufanyika nchini Korea Kusini na Japani.[3] Mashindano haya yatakuwa ya mwisho yakihusisha jumla ya timu 32.

Ufikapo mwaka 2026 kutakuwa na ongezeko la jumla ya timu 48. Mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ilikuwa timu ya taifa ya Ufaransa. [4] Kutokana na majira ya joto nchini Qatar, Kombe hili la Dunia litafanyika kuanzia 20 Novemba hadi 18 Desemba 2022, na kufanya kuwa mashindano ya kwanza kutokufanyika katikati ya mwaka kati ya mwezi Mei, Juni, au Julai.

  1. Elias, Jaan; Mobarak, Mushfiq; Rosenthal, Jean (2020). Qatar FIFA World Cup 2022. 1 Oliver's Yard, 55 City Road, London EC1Y 1SP United Kingdom: Yale School of Management. ISBN 978-1-5297-9640-7. {{cite book}}: no-break space character in |location= at position 17 (help)CS1 maint: location (link)
  2. "Amir: 2022 World Cup Qatar a tournament for all Arabs", Gulf Times, 15 July 2018. 
  3. Taylor, Daniel (15 Julai 2018). "France seal second World Cup triumph with 4–2 win over brave Croatia". The Guardian. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Juni 2019. Iliwekwa mnamo 7 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "FIFA Executive Committee confirms November/December event period for Qatar 2022". FIFA. 19 Machi 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2017. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search